Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya tairi za gari.
Usafiri ni hitaji muhimu la wanadamu. Sekta ya usafiri huwa inakua kadiri idadi ya watu inavyoongezeka.
Sekta hii inatoa fursa mbalimbali za mtu kuingia na kutengeneza kipato.
Moja ya fursa hizo ni uuzaji wa tairi za magari.
Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia uuzaji wa tairi za magari.
- Kununua tairi mpya kwa jumla na kuuza kwa reja reja.
-
Kuwa wakala wa makampuni ya tairi na kuuza kwa jumla.
-
Kununua na kuuza tairi ambazo zimeshatumika ila zipo kwenye hali nzuri.
-
Kuwa na eneo la kubadili tairi na kuziba pancha.
-
Kuwa na matawi mbalimbali ya uuzaji wa tairi za magari.
-
Kufungua maeneo mbalimbali ya kubadili tairi na kuziba pancha.
-
Kuwa mshauri wa mambo yanayohusu tairi, hasa kuchagua ubora na matunzo mazuri.
-
Kukusanya na kuuza tairi chakavu kwa matumizi mbadala kama urembo au kutengeneza viatu.
-
Kuuza bidhaa na huduma nyingine zinazoendana na tairi kama rim na urembo mwingine wa tairi.
-
Kutangaza tairi mbalimbali kupitia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii.
Kocha.