2376; Vinavyozuia Biashara Kukua…
Kwa asili, kitu chochote kinachozaliwa kinapaswa kukua.
Na kama hakikui basi kuna sababu, kuna kitu kinazuia.
Kama mtoto amezaliwa na hakui, haongezeki uzito, hukai na kuridhika, lazima ujue sababu ni nini na kuchukua hatua.
Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwenye biashara pia.
Biashara inapoanzishwa, inapaswa kukua.
Kama haikui kuna vikwazo vinaizuia.
Hapa ni baadhi ya vikwazo ambavyo vipo kwenye biashara nyingi.
- Hakuna mtaji wa kutosha unaozunguka kwenye biashara. Hivyo hata kama fursa zipo, haziwezi kufanyiwa kazi.
-
Mauzo yanayofanyika kwenye biashara ni kidogo na hivyo hakuna fedha ya kutosha inayoingia.
-
Hakuna wateja wa kutosha kwenye biashara na hilo linaathiri mauzo.
-
Bei inayotozwa kwa wateja siyo ya kutosha kuweza kutengeneza faida nzuri.
-
Gharama za kuendesha biashara ni kubwa na hizo zinachukua faida yote.
-
Huna mfumo mzuri wa kuiendesha biashara kiasi cha kutokukitegemea moja kwa moja.
-
Hakuna vipaumbele sahihi kwenye biashara.
-
Wazo au muundo wa biashara siyo sahihi kwa mazingira au wakati.
Ukitatua hayo maeneo, biashara lazima itakua vizuri.
Kocha.