Maendeleo na hatua zote ambazo tumepiga kama binadamu, ni kwa sababu ya mamba.

Uwezo wa kupima na kulinganisha vitu umekuwa msukumo mkubwa kwetu kufanya vitu kwa utofauti mkubwa.

Bila ya namba ni rahisi kujidanganya na kuamini unafanya makubwa. Lakini namba hazidanganyi, kama kitu kimefanyika kinaweza kupimika.

Weka imani yako kwenye namba na siyo hadithi, tumia namba kwenye kufanya maamuzi yote muhimu kwako. Namba hazikubembelezi, zinakuonyesha ukweli ulivyo.

Ukurasa wa kusoma ni kitu kimoja unachopaswa kuamini; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/16/2389

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma