2392; Unavyojitengenezea Maumivu…
Sehemu kubwa ya maumivu unayopitia kwenye maisha yako, huwa unayatengeneza wewe mwenyewe.
Unafanya hivyo bila ya kujua.
Hapa ni baadhi ya mambo ambayo umezoea kufanya ambayo yanakuweka kwenye hatari ya kupata maumivu.
- Kuwa na matarajio makubwa kwenye vitu usivyokuwa na udhibiti navyo.
-
Kulazimisha matokeo ya aina fulani.
-
Kutaka kumfurahisha au kumridhisha kila mtu.
-
Kukosa umakini kwenye kile unachofanya.
-
Kuishi kwa maigizo badala ya uhalisia.
-
Kutegemea mambo yawe rahisi.
Kujitambua na kuwa wewe, kuwa tayari kuukabili ukweli na kuweka umakini wako wote kwenye kile unachofanya itakusaidia kuondoa maumivu ya kujitengenezea.
Kocha.