Ni watu ambao hupaswi kuwaruhusu wakusumbue kwa namna yoyote ile.

Kwa sababu mtu akiwa na chuki na wewe, tayari ana chuki na yeye binafsi.

Hakuna namna unaweza kumlazimisha anayekuchukia akupende, maana yeye mwenyewe hajipendi.

Watu wanaojipenda hawana muda wa kuwa na chuki kwa wengine.

Na watu wenye chuki, hawana manufaa yoyote kwa wengine.

Wapuuze wenye chuki, komaa na wale wanaoelewa unachofanya na wanaonufaika nacho pia, hayo ndiyo matumizi bora ya nguvu na muda wako ambazo ni rasilimali zenye uhaba.

Ukurasa wa kusoma leo ni kutaka kupendwa na kila mtu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/18/2391

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma