
Usiunganishe moja kwa moja maamuzi unayofanya na matokeo unayopata.
Maamuzi sahihi yanabaki kuwa sahihi hata kama matokeo yake ni tofauti na ulivyotarajia.
Usikimbilie kubadili maamuzi kwa sababu matokeo siyo mazuri, badala yake badili mbinu unazofanyia kazi.
Kuwa na mchakato wa kufikia maamuzi sahihi na pia kuwa na mchakato wa kufanyia kazi maamuzi hayo na pambana na mchakato na siyo matokeo.
Huna udhibiti kwenye matokeo, bali una udhibiti kwenye maamuzi na mchakato, tumia udhibiti huo vizuri.
Ukurasa wa kusoma ni usibadili maamuzi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/25/2398
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma