Unayashindwa maisha, kazi au biashara kabla hata hujaanza kwa sababu unawaiga wengine.

Unapofanya kama wanavyofanya wengine, watu wanakuwa hawana sababu ya kuja kwako. Unakuwa umewaambia kwamba wewe huna umuhimu wowote.

Njia pekee ya kushinda ni kuwa wewe, wewe ambaye ni wa kipekee, ambaye hujawahi kutokea na hutakuja kutokea tena.

Weka upekee wako kwenye kila unachofanya na zalisha thamani ya tofauti ambayo inawavuta watu kuja kwako kwa sababu wanachopata kwako hawawezi kukipata kwa mwingine yeyote.

Ukurasa wa kusoma ni kujenga nguvu ya ushindani; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/26/2399

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma