Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kufanya usafi.

Usafi ni hitaji muhimu la kila mwanadamu, hasa kwa mazingira na mwili wake.

Lakini siyo watu wote wana muda wa kufanya usafi wao wenyewe.
Hivyo wanatoa fursa kwa watu kuweza kuingiza fedha kupitia ufanyaji wa usafi.

Hapa ni mawazo 10 ya kuweza kufanya hivyo.

  1. Kuwa na kampuni ya kufanya usafi na kuwafikia wateja kule walipo.

  2. Kutoa mafunzo kwa wafanya usafi na wakalipia.

  3. Kuuza bidhaa mbalimbali za kufanyia usafi.

  4. Kuwa wakala wa bidhaa za usafi.

  5. Kuwa na gari linalozunguka kutoa huduma za usafi.

  6. Kuandikisha watu ambao utakuwa unawafanyia usafi na wao kulipa kila mwezi.

  7. Kuandika vitabu na makala kuhusu usafi na watu kulipia kuvipata.

  8. Kutengeneza video za njia mbalimbali za kufanya usafi na kuweka YouTube kisha kuingiza kipato kwa matangazo.

  9. Kuwa na tanuru maalumu la kuteketeza taka na watu wakalipia kulitumia.

  10. Kuwa na tovuti au app inayowakutanisha watoaji wa huduma za usafi na wahitaji wa huduma hizo. Mfano mtu anapohitaji huduma ya usafi, anaongia na kuweka hitaji lake, kisha mtoa huduma aliye karibu anampatia huduma hiyo.

Kocha.