Kuna mtu mmoja tu unayeweza kumridhisha na kumfurahisha kwenye maisha yako. Mtu huyo ni wewe mwenyewe.

Utajiridhisha kwa kuishi maisha ya kweli kwako na siyo kuishi maisha ya maigizo ili kuwaridhisha wengine.

Haijalishi unafanya nini, wapo watu watakaokuona wewe ni takataka na hufai kabisa. Siyo kwa sababu yako, bali kwa sababu zao wenyewe.

Hivyo usiruhusu watu wa aina hiyo wakuvuruge, wewe ishi maisha ya kweli kwako.

Ukurasa wa kusoma leo ni watu kukuona takataka; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/29/2402

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma