2410; Hupati Muda…
Kama unajiambia ukipata muda utafanya kitu, jua ni njia tu ya kujifanganya.
Ukweli unaopaswa kujiambia ni kitu hicho siyo muhimu sana kwako na hivyo hakipaswi kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.
Maana kitu kinapokuwa muhimu kabisa huwa hatusubiri mpaka tupate muda, badala yake tunatenga muda.
Hivyo acha kujidanganya, pale unapojiambia huna muda au ukipata muda utafanya kitu, jikamate na ujiambie huo ni uongo.
Jiambie tu ukweli kwamba kitu hicho siyo muhimu na kinachostahili kupewa kipaumbele cha kwanza kwako.
Hupati muda bali unatenga muda.
Kama kitu ni muhimu kwako, husubiri mpaka upate muda, bali unakitengea muda.
Tenga muda wa yale muhimu kufanya na hutasumbuka na yasiyokuwa muhimu.
Kocha.