Rafiki yangu mpendwa,
Hizi teknolojia mpya ambazo zimekuja sasa, hasa mitandao ya kijamii, zimetupa kazi mara mbili.

Kila mtu anayetumia mitandao ya kijamii anakazana kuongeza zaidi wafuasi ambao anao.
Wengi wamekuwa wakienda mbali katika hilo na kuomba watu ‘wawa-follow’ au hata kununua followers.

Kazi nyingine kubwa ambayo watu wanajipa kwenye hiyo mitandao ni kupata ‘likes’ nyingi.
Watu hukazana ‘kupost’ vitu ambavyo vitawafanya wafuasi wao ‘wa-like’ zaidi.

Mitandao hii ya kijamii imekuwa inamsukuma kila mtumiaji atafute umaarufu kupitia idadi ya ‘followers’ na ‘likes’.

Hakuna ubaya wowote kwenye hilo, ila swali la msingi ni je unaingiza fedha kwa hayo mambo unayohangaika nayo?
Kama jibu ni huingizi fedha, basi jua kwamba mitandao hiyo imekugeuza wewe kuwa bidhaa.

Inakugeuza kuwa bidhaa kwa kukufanya uitumikie, utumie muda wako mwingi kwenye mitandao hiyo na uwalete wengine wengi nao watumie muda wao mwingi.

Hivyo ndivyo mitandao ya kijamii inavyotengeneza faida kubwa na kuwafanya wamiliki wake kama wakina Mark Zuckerberg kuwa matajiri wakubwa duniani.

Uzuri ni kwamba, zipo njia ambazo unaweza kuanza kuzitumia mara moja na ukaingiza fedha kwa kupitia wafuasi unaowajenga kwenye mitandao ya kijamii.

Njia hizo zimefanywa ni siri na kufichwa, ili kufanya mamilioni ya watumiaji wa mitandao hiyo ya kijamii kuendelea kuwa bidhaaa kwa wamiliki.

Je wewe unataka kuacha kuwa bidhaa kwenye mitandao na uanze kuitumia kwa faida?
Kama jibu ni ndiyo basi nikupongeze, umefika mahali sahihi, kwani leo unapata nafasi ya kujifunza hilo na kuweza kuchukua hatua mara moja.

Siri nzima ya hili inapatikana kwenye kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU.
Kitabu hiki kinakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kujenga wafuasi sahihi na wanaokuamini kweli (true fans) ambao wapo tayari kununua chochote kile unachouza.

Moja ya sura kwenye kitabu inaelezea mchakato wa 1, 10, 100 na 1000. Hizo ni namba muhimu za kufanyia kazi hatua kwa hatua na kuyapata matokeo mazuri mno.

Njia nyingi ambazo watu wanahangaika nazo sasa kuingiza kipato kupitia wafuasi wa mtandaoni siyo sahihi.
Kwa sababu hawajui jinsi ya kujenga wafuasi sahihi watakaokuwa tayari kununua kila wanachouza.

Pata leo na usome kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili ujifunze njia sahihi na uanze kuitumia mara moja na utanufaika sana.

Rafiki, hiki siyo kitabu cha kukosa kama unataka kuongeza kipato chako zaidi.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.

Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.

Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; http://www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.

Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf

Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz