2422; Siyo kweli..

Siyo kweli kwamba umeshafanya kila kinachowezekana kufanyika, kuna vingi hujafanya, hivyo endelea kufanya.

Siyo kweli kwamba umeshamfikia kila mtu, kuna wengi hujawafikia, endelelea kuwafikia wengi zaidi.

Siyo kweli kwamba kila kitu kimeshasemwa, bado dunia haijasikia sauti yako.

Siyo kweli kwamba huna muda, hujaupangilia tu vizuri.

Chochote unachojiambia kama sababu ya kukosa unachotaka, ni kujidanganya tu.

Kama bado hujapata unachotaka, wajibu wako na kipaumbele cha kwanza kwako ni kupata hicho unachotaka.

Mengine yote nje ya hapo siyo kweli, ni kujidanganya tu.
Hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa kujidanganya.

Kila unapojipa sababu, jiambie mara moja siyo kweli, kisha endelea na safari.

Kocha.