
Watu wapo tayari kukupa kila aina ya ushauri hata kama hujawaomba.
Watakupa ushauri huo bure kabisa na kukuonyesha kwamba ni muhimu kwako. Wengine wataenda mbali zaidi na kukulaumu kama hutafanyia kazi ushauri wao.
Lakini kama tunavyojua, hakuna kitu cha bure, ushauri wa bure una gharama kubwa ambayo ni kukutoa kwenye ndoto yako kubwa.
Yeyote anayekushauri kabla hujamweleza kwa kina nini hasa unataka, anakushauri vitu ambavyo haviendani na ndoto yako kubwa.
Hivyo usikimbilie kufanyia kazi ushauri wa bure unaopewa, upime kwanza kama unaendana na ndoto zako kubwa.
Ukurasa wa kusoma ni siyo kila ushauri unakufaa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/17/2421
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma