
Kama umewahi kudanganywa, kuibiwa au kutapeliwa, ni kwa sababu kuna umakini ambao uliukosa.
Watu huwa wanadanganya kwa maneno, lakini vitendo vyao huwa wazo kabisa.
Ukiwa makini, lazima utaona tofauti kati ya unachosikia na unachoona.
Mtu anakuambia kuna fursa yenye manufaa mahali, wakati ukimuangalii hafananii na mwenye kujua fursa ya aina hiyo.
Pale unaposikia na unachoona vinapopingana, amini kile unachoona.
Ukurasa wa kusoma ni unachoona na unachosikia; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/22/2426
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma