
Kila mteja unayemhudimia, mchukulie ndiye mteja wa kwanza kwako na wa kipekee kabisa. Kwa sababu hivyo ndivyo mteja anavyojichukulia.
Wewe unaweza kuwa umeshawahudumia wateja wengi na umechoka, ila mteja mwingine anapokuja hajui wala kujali yote hayo.
Ukimpa huduma mbovu hataangalia umehudumia wateja wangapi vizuri, yeye atakachojua ni kimoja, hujamhudumia vizuri na hata kama hatakuambia, majibu utayaona, hatarudi tena kwako.
Tunapaswa kuweka umakini mkubwa kwenye eneo la huduma kwa wateja, kwani mambo madogo madogo yana nguvu kubwa sana.
Soma zaidi kwenye ukurasa huu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/25/2429
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma