Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio ya kitu chochote kile yanategemea sayansi na sanaa.
Wengi wanashindwa kwa sababu huwa wanaegemea upande mmoja, labda sayansi pekee au sanaa pekee.

Ili upate mafanikio kwenye jambo lolote, lazima uwe na mlinganyo sahihi kwenye sayansi na sanaa ya kile unachofanya.

Kabla hatujaona jinsi ya kutumia sayansi na sanaa kwenye biashara, kwanza tujue maana ya maneno hayo mawili.

Sayansi ni kitu ambacho kinaweza kurudiwa na kuleta majibu yake yale. Kwa kifupi sayansi ina kanuni, ambayo ikifuatwa kwa usahihi, matokeo yanajulikana kabisa.

Sanaa ni kitu ambacho hakiwezi kurudiwa na kuleta majibu yale yale. Sanaa haina kanuni, mtu anaweza kufanya kile kile na bado akapata majibu ya tofauti kabisa.

Sayansi na sanaa kwenye biashara.

Biashara ina pande mbili, sayansi na sanaa.

Upande wa sayansi ni ule wenye kanuni na miongozo ambayo inapaswa kufuatwa ili biashara ifanikiwe.

Mfano ni mfumo wa biashara, namba za biashara, mzunguko wa fedha kwenye biashara na mikakati ya masoko na mauzo.

Hivyo vitu lazima vifanyiwe kazi kwa usahihi na umakini mkubwa ili biashara iweze kufanikiwa.

Upande wa sanaa ni ule ambao hauna kanuni wala miongozo, huu unatokana zaidi na machale na uzoefu wa mtu.

Sanaa ni muhimu sana kwenye kuchaguwa watu wa kushirikiana nao. Hakuna kanuni unayoweza kutumia kupata watu sahihi, ni kitu kinachotegemea machale na uzoefu binafsi.

Eneo jingine la sanaa kwenye biashara  ni bahati.  Kila biashara iliyofanikiwa imekutana na bahati fulani katika kipindi chake.
Japo bahati hizo zinaweza kutengenezwa, hakuna kanuni ya uhakika ambayo ukiifuata utatengeneza bahati. Ni kitu kinachotegemea zaidi machale na uzoefu binafsi.

Ubunifu ni eneo jingine la sanaa kwenye biashara. Hakuna kanuni ya ubunifu, ni namna mtu anachangamana na mazingira yake na kuangalia yale yanayoendelea ndiyo anaweza kuja na ubunifu mzuri.

Mwaka wa mafanikio 2021/2022 ni kufanya biashara kwa sayansi na sanaa.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo ni hitimisho la mwaka wa mafanikio 2020/2021 na kuanza kwa mwaka wa mafanikio 2021/2022 tunakwenda kupata nafasi ya kujifunza kwa kina jinsi ya kuendesha biashara zetu kisayansi na kisanaa.

Tutajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza mfumo wa biashara na kuzifuatilia namba za biashara yako kwa uhakika kabisa.

Halafu tutajifunza jinsi ya kufikiri kama mjasiriamali, kitu kinachokuweka kwenye hali ya kuiendesha biashara yako kisanaa na ikanufaika sana.

Kwa kuunganisha pande hizo mbili za biashara, itaweza kukua kwa kasi na kuwaacha mbali washindani ambao wanaendesha biashara zao kwa mazoea tu.

Karibu sana kwenye semina, uje ukiwa na mpango wako wa biashara ili tuusuke vizuri na uende ukaufanyie kazi kwa mafanikio makubwa.

Usikubali kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itafanyika jijini Dodoma tarehe 16 na 17 Oktoba 2021.
Kama bado hujathibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717 396 253.

Pia kwenye semina hiyo tunakwenda kutengeneza mfumo mzuri wa kuwajibishana kwenye biashara, kitu kitakachokusukuma ukae kwenye mipango yako na ujitume sana.

Kama unataka kuwa sehemu ya mfumo huo wa uwajibikaji, fungua na ujaze fomu kwenye kiungo ninachoweka hapa. Kama umeshajaza fomu usirudie tena.
Kiungo cha kujaza fomu ni hiki; https://bit.ly/kisimainfo

Rafiki, kuwa mwanasayansi na msanii katika kuiendesha na kuikuza zaidi biashara yako.
Karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili tukajenge msingi kwenye hilo.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
www.somavitabu.co.tz