2431; Kuchinja kuku anayetaga…

Ili upate mayai zaidi ni jambo la ajabu lakini ambalo limekuwa linafanywa na wengi.

Wengi huanza na kitu chini kabisa, wanaweka juhudi kubwa na hizo kupelekea kitu hicho kuwapa matokeo mazuri.

Wakishapata matokeo mazuri wanajisahau na kujikuta wanaharibu kabisa kile kilichokuwa kinawapa matokeo hayo.

Kinachotokea ni wanayakosa matokeo waliyokuwa wanayapata na hilo linakuwa chanzo cha anguko.

Haijalishi umepiga hatua kiasi gani, usisahau kile kilichokusaidia kupiga hatua hizo.

Huwa ni rahisi kusahau kile kilichokufikisha pale ulipo sasa, lakini usilipe hilo nafasi kabisa.
Endelea kusimamia kile kilichokupandisha ili uweze kupanda juu zaidi.

Mafanikio kidogo unayopata yasigeuke kuwa kikwazo kwako kupata mafanikio makubwa zaidi.

Endelea kuweka juhudi kwenye kile kikichokufikisha juu ili uende juu zaidi.

Jikumbushe hili, usichinje kuku anayetaga kwa tamaa ya kupata mayai mengi kwa wakati mmoja.

Endelea kumtunza kuku wako vizuri ili aendelee kukupatia mayai.

Kuna wakati tamaa ya kupata mafanikio makubwa na ya haraka inakuwa chanzo cha kuharibu kabisa mafanikio yako.

Ujue wakati huo na uepuke ili mafanikio yako yasivurugike.

Kocha.