
Kutaka mambo yaende kama unavyotaka wewe na kuona hayawezi kwenda tofauti na hivyo ni kujiandaa kuumia.
Kwa sababu dunia haipeleki mambo yake kwa kuangalia matakwa ya watu, bali inatumia kanuni zake yenyewe.
Unachoweza kudhibiti wewe ni juhudi unazoweka na mchakato unaofanyia kazi. Kwa upande wa matakeo, yatakuja yenyewe kwa namna yake na siyo kwa matakwa yako.
Hivyo wewe unapaswa kujiandaa kwa matokeo ya aina yoyote huku ukijua hata yatokee matokeo ya aina gani, bado utakuwa kwenye nafasi ya kuendelea na mapambano, maana hicho ndiyo muhimu zaidi, kuendelea na mapambano.
Mwisho wa siku kuna mtu atakutaba na bahati na fursa nzuri, lakini atakuwa yule anayeendelea na mapambano, hakikisha unakuwa wewe.
Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/26/2430
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma