Sisi binadamu huwa tunazoea vitu haraka, kisha tunavichoka na kutaka kuvibadilisha. Tunapenda vitu vinavyotusisimua na kuibua hisia zetu.

Ni katika harakati hizo ndiyo tunajikuta tumeharibu au kupoteza kile kilichokuwa na manufaa kwetu huko nyuma.

Unapaswa kuwa makini sana kwenye hili, kwa kuhakikisha unalinda kila ambacho kina manufaa kwako ili usikiharibu kwa mahangaiko yako.

Usichinje kuku anayetaga kwa sababu umechoka kupata yai moja tu kila siku. Kwa kumchinja unaweza kupata mayai mengi kwa pamoja, lakini huo unakuwa ndiyo mwisho wa kupata mayai kutoka kwa kuku huyo.

Heshimu sana kile kinachokupa matokeo mazuri na endelea kukitunza na kukitumia vizuri.

Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/27/2431

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma