2433; Kichekesho cha jamii…

Mchekeshaji mmoja amewahi kusema watu wanatumia fedha ambazo hawana, kununua vitu ambavyo hawavitaki ili kujionyesha kwa watu ambao hawajali.

Na mwandishi Morgan Housel kwenye kitabu chake cha psychology of money ameandika kuhusu dhana ya mtu aliye kwenye gari la kifahari.
Anasema wengi hununua magari ya kifahari ili waonekane na wengine.
Wakati watu wanapoyaona magari hayo ya kifahari, hawawafikirii sana wamiliki, bali wanajifikiria wao wenyewe siku wanayoweza kuja kumiliki magari kama hayo.

Kwa kifupi ni ishi maisha yako, hakuna anayejali sana kuhusu maisha yako kama unavyodhani.
Kila mtu tayari amevurugwa na maisha yake, hakuna mwenye nafasi ya kutosha na kuyabeba maisha yako pia.

Kocha.