Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi cha juma cha ONGEA NA KOCHA.

Kwenye kipindi hiki unakwenda kupata yafuatayo;

Moja ni somo la wewe ni mshindi, ambapo nimekushirikisha kwa kina namna ya kufikiri kama mshindi, kufuta kabisa mbadala na kupambana mpaka ufanikiwe.

Mbili ni uchambuzi wa kitabu cha Third Door ambapo mwandishi ameshirikisha njia mbadala ambayo wale waliofanikiwa sana walizitumia katika kuanza safari yao ya mafanikio.

Tatu ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Ernest Paschal ambaye anatushirikisha safari yake ya mafanikio aliyopitia maanguko mengi ila akawaza kuinuka na kuendelea na mapambano.

Nne ni mjadala wa pamoja wa wanamafanikio wote ambapo wameshirikisha waliyojifunza pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kutokana na yale yaliyoendelea kwenye kipindi.

Fungua kipindi usikilize, ujifunze na kwenda kuchukua hatua ili maisha yako yawe bora zaidi.

Kocha.