#SheriaYaLeo (29/366); Kuwa jinsi ulivyo.
Unapaswa kuwa jinsi ulivyo kwa kujifunza wewe ni mtu wa aina gani, kisha kuwa mtu huyo.
Ulizaliwa na uwezo, tabia na vipaji vya kipekee ambavyo vinakutofautisha na wengine na kujenga hatima yako. Hivyo ndivyo ulivyo ndani yako.
Ni kwa kuishi huo upekee wako ndiyo unaweza kufanya makubwa sana hapa duniani.
Kwa bahati mbaya sana, wengi huwa hawawi jinsi walivyo, hawaishi upekee wao.
Wanaishia kuiga maisha ya wengine na kuficha upekee wao ambao ndiyo wenye nguvu kubwa.
Hilo linawafanya waishie kuwa watu wa kawaida na wasiweze kufanya makubwa.
Sheria ya leo; Jijue wewe ni mtu wa aina gani kwa kuweka umakini kwenye sauti na nguvu zilizo ndani yako. Kwa njia hiyo utaweza kuwa yule ambaye uliandaliwa kuwa na kufikia ubobezi mkubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu