#SheriaYaLeo (31/366); Chanzo cha nguvu zote.

Usijaribu kuikwepa kazi ya kugundua kusudi na wajibu wa maisha yako kwa kudhani vitakuja kwako vyenyewe.
Japo inaweza kutokea hivyo kwa baadhi ya watu, kuweza kujua kusudi na wajibu wa maisha yao mapema na kwa matukio ya kipekee, kwa wengj wetu hilo linahitaji kazi na muda.

Inatutaka kujitafakari kwa kina ndani yetu huku tukijaribu ujuzi wa aina mbalimbali kulingana na yale tunayopendelea kufanya.

Kuwa tayari kuweka juhudi hizo kubwa na kwa muda mrefu bila kuchoka ndiyo hatua muhimu sana ya kujua kusudi na wito na kuweza kufikia ubobezi wa hali ya juu.

Sheria ya leo; Kujijua wewe mwenyewe kwa undani na upekee wako kutafanya rahisi kwako kuepuka makosa mbalimbali kwenye maisha. Chanzo cha nguvu zote ni kujitambua wewe mwenyewe.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu