#SheriaYaLeo (37/366); Jichukulie Kama Mjenzi.

Haijalishi upo kwenye tasnia gani, unapaswa kufikiri na kujichukulia kama mjenzi.
Wewe ni mjenzi unayetumia rasilimali na mawazo mbalimbali kutengeneza kitu chenye manufaa kwa wengine.

Kujenga kitu chochote vizuri, iwe ni nyumba, taasisi, biashara au kazi ya sanaa, ni lazima uuelewe mchakato wa ujenzi na kuwa na ujuzi sahihi wa kuweza kufanya hivyo.

Unaweza kupata ujuzi huo kupitia kupata mafunzo ya karibu kutoka kwa wale ambao tayari wameshabobea.
Kama ambavyo fundi seremala anajifunza kutoka kwa fundi seremala mwingine, ndivyo pia unapaswa kujifunza ujenzi wako kutoka kwa waliobobea.

Huwezi kutengeneza kitu chochote cha thamani hapa duniani bila kwanza ya kujibadili na kujiendeleza wewe mwenyewe.

Sheria ya leo; Kama mjenzi, jiwekee viwango vya juu kabisa na kuwa na uvumilivu wa kukaa kwenye kila hatua ya mchakato mzima wa ujenzi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu