#SheriaYaLeo (41/366); Jifunze Kutoka Kwenye Kila Kitu.

Kila jukumu unalopewa au kuwa nalo linakupa fursa ya kujifunza kuhusu kile unachofanya, watu na dunia kwa ujumla.

Hakuna jukumu ambalo halina fursa hiyo ya kujifunza na hakuna taarifa ndani ya kitu ambazo ni ndogo na zisizo na uzito.

Kila kitu unachosikia au kuona ni kiashiria unachopaswa kuking’amua.
Kadiri unavyong’amua kila unachokutana nacho ndivyo unavyoelewa kwa kina unachofanya, watu na dunia kwa ujumla.

Kwa kujifunza huko, kadiri muda unavyokwenda unaanza kuelewa mambo ambayo yalionekana magumu kwako.
Kwa mfano mtu uliyedhani ana mamlaka makubwa unakuja kugundua ni maneno tu, ndani hana mamlaka yoyote.

Taratibu taratibu unaanza kuona na kuelewa yale yaliyojificha nyuma ya pazia.
Kadiri unavyokusanya taarifa nyingi ndiyo unapata uelewa kwa nini mambo yapo na yanaenda vile yanavyoenda.
Na hapo ndipo unaweza kujua kipi sahihi unapaswa kufanya katika hali za namna hiyo.

Sheria ya leo; Kabili kila jukumu, hata ambalo ni dogo kiasi gani kwa namna sawa; kama fursa ya kujifunza na kukusanya taarifa za kutosha kuhusiana na kitu husika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu