#SheriaYaLeo (42/366); Jinsi ya kujifunza kwa kasi.
Kwa chochote unachojifunza, unajifunza kwa kasi zaidi kupitia kufanya kuliko kupitia kusoma au kusikiliza maelekezo.
Mwanzo wa kufanya huwa ni mgumu, lakini kadiri unavyoendelea kufanya ndivyo inavyokuwa rahisi.
Unajifunza kwa kasi na ubora zaidi kwa kufanya kile unachojifunza.
Hata kama ni lugha mpya unajifunza, unaweza kuisoma sana, lakini hutajifunza kwa kasi kama hutaizungumza lugha hiyo.
Unapofanya kwa kurudia rudia inazidi kuwa rahisi kwako na unajijengea ubobezi mkubwa.
Unapofanya kitu kwa muda mrefu unajenga mapenzi nacho zaidi, unakijua kwa undani zaidi na kuzidi kukifanya kwa viwango vya juu zaidi.
Lengo lako kwa chochote unachojifunza ni kufika hatua hiyo ya kujifunza kwa kasi, kupitia kufanya kwa kurudia rudia.
Sheria ya leo; Chochote chenye thamani kufanya huwa kina hatua za kujifunza. Pale kinapokuwa kigumu, kumbuka lengo lako ni kufikia kujifunza kwa kasi ambapo kunatokana na kufanya kwa kurudia rudia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu