2543; Zima Washa.
Kifaa chochote cha kielektroniki kikikusumbua, kabla hujapeleka kwa fundi, huwa unashauriwa kufanya kitu kimoja, kukizima kisha kukiwasha (restart).
Iwe ni siku, redio, tv, kompyuta na vinginevyo, zoezi la kuzima na kuwasha huwa linatatua sehemu kubwa ya matatizo.
Mara nyingi vifaa hivyo hukaa sawa baada ya kuzima na kuwasha.
Kwa bahati nzuri ni kwamba hilo pia huwa linafanya kazi kwetu binadamu.
Pale unapokuwa hujielewi elewi, kabla hujahangaika na mambo mengine, kwanza jizime na ujiwashe, kwa maana ya kulala na uamke.
Kwa kupata muda wa kutosha wa kulala, mwili wako hufanya marekebisho mbalimbali. Hivyo unapoamka vitu vingi vinakuwa sawa.
Hata pale unapokuwa unajaribu kufikiria kitu na hupati majibu, usiendelee kujilazimisha, badala yake lala na uamke, utashangaa jinsi majibu yatakavyokuja kwako kiurahisi.
Hatua ya kuchukua;
Pale unapokuwa huuelewi mwili na akili yako, kabla hujahangaika na vitu vingine, hakikisha kwanza huna njaa, huna kiu na huna usingizi.
Hivyo anza kwa kula, kunywa maji ya kutosha na kulala.
Ukiamka, mambo yatakuwa tofauti.
Tafakari;
Kuna wakati miili yetu inachoka lakini hatuelewi hilo. Zoezi la kulala na kuamka linatatua sehemu kubwa ya matatizo ya mwili na akili tunayokuwa nayo.
Kocha.
Asante Sana kocha kwa hili, zima washa ni njia bora ya kupata ufumbuzi wa matatizo yetu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike