#SheriaYaLeo (47/366); Jifunze na kufanya kwa kina.
Watu wengi huwa wanajifunza na kufanya vitu kwa juu juu.
Huwa wanataka yale maeneo ya kufurahisha na kusisimua.
Lakini hivyo sivyo ubobezi unavyojengwa.
Ubobezi unajengwa kwa kujifunza na kufanya kwa kina.
Kujifunza na kufanya kwa kurudia rudia yale ya kawaida na yanayochosha.
Hayo ndiyo yanakujengea msingi sahihi ambao unakufikisha kwenye ubobezi.
Achana na mazoea na urahisi wa kupenda vitu vya juu juu na rahisi.
Jitoe kujifunza na kufanya vitu kwa kina na hilo litakuwezesha kufika kwenye ubobezi wa hali ya juu.
Sheria ya leo; Bobea kwenye yale ya msingi kabisa na mengine yatajiweka mahali pale.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu