2552; Mkia wa mbuzi.
Mkia wa kondoo huwa unazifunika nyeti zake, kwa njia hiyo mkia unakuwa na manufaa kwake.
Mkia wa ng’ombe huwa unamwezesha kufukuza inzi kwenye mwili wake, na hivyo kuwa na manufaa kwake.
Lakini mkia wa mbuzi, huwa hauna manufaa yoyote, hauwezi kufunika nyeti zake na wala hauwezi kufukuza inzi kwenye mwili wake.
Japo unaonekana ni mkia, lakini hauna matumizi kwake.
Kwenye maisha, kuna vitu ambavyo tunang’ang’ana navyo lakini havina manufaa makubwa kwetu.
Japo vitu hivyo vinaonekana kuwa na manufaa kwa wengine, hata ukae navyo kwa muda mrefu kiasi gani, havitakuwa na manufaa kwako.
Hatua ya kuchukua;
Fikiria kwenye maisha yako ni vitu gani unang’ang’ana navyo kwa sababu umeona vina manufaa kwa wengine ila havina manufaa kwako. Ni wakati sasa wa kuachana na vitu hivyo kwa sababu haijalishi utang’ang’ana navyo kwa muda mrefu kiasi gani, havitakuwa na manufaa kwako kwa sababu tu vina manufaa kwa wengine.
Tafakari;
Siyo kila chenye manufaa kwa wengine kinaweza kuwa na manufaa kwako pia.
Siyo kila ambacho ni fursa kwa wengine kinaweza kuwa fursa kwako.
Tathmini kila kitu kwa namna ambavyo kina manufaa kwako na siyo kuangalia tu kwa wengine.
Kocha.