#SheriaYaLeo (70/366); Maarifa ndiyo ukuu wako.

Maarifa kidogo ni sumu kubwa.
Kwa kujua kidogo unaweza kupata kiburi na kudhani tayari unajua kila kitu.
Unachopaswa kujua ni kwamba maarifa yanaendelea kubadilika kadiri muda unavyokwenda.

Historia iko wazi kabisa, vitu vingi ambavyo watu waliamini ni kweli, kwa sasa vimethibitishwa siyo kweli.
Maendeleo ya sayansi yanatupa nguvu ya kupima kila maarifa yaliyopo kuona kama ni kweli au la.

Hivyo badala ya kuwa na kiburi kwa maarifa uliyonayo na kudhani umeshajua kila kitu, unapaswa kuwa mnyenyekevu na kujua hata unayojua yanaweza yasiwe sahihi kama unavyodhani.
Jua chochote kinachoaminika kuwa kweli leo, kinaweza kuthibitishwa siyo kweli siku zijazo.

Na hili ndiyo linatofautisha dini na sayansi. Sayansi ina mfumo mzuri wa kujirekebisha yenyewe, hivyo maarifa yanapothibitishwa siyo kweli, inakuwa tayari kubadilika.
Lakini dini huwa zinasimamia kitu kile kile, hata kama imethibitishwa siyo kweli bado hazibadiliki, maana zinasimamia kwenye kuamini zaidi kulilo kutafuta ukweli.

Sheria ya leo; Maarifa yanapiga hatua mara zote, chochote ambacho ni kweli leo, kesho kinaweza kisiwe kweli. Usiruhusu kiburi chako kikupoteze, maarifa ndiyo ukuu wako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu