#SheriaYaLeo (71/366); Weka umakini mkubwa.

Ili kufikia ubobezi wa hali ya juu, unapaswa kuweka umakini mkubwa sana kwenye chochote kile unachoamua kufanya.

Usifanye tu kwa juu juu au kwa mazoea, badala yake fanya kwa kina kabisa.
Jua undani wa kile unachokifanya na kifanye kwa namna ya tofauti na ya kipekee kabisa.

Usifanye kwa sababu ndivyo wengine wanafanya.
Na wala usifanye leo kama ulivyofanya jana.

Bali kila unapofanya, kuwa kama unafanya upya.
Kila unachokutana nacho, kitumie kama sehemu ya kujifunza kwa kina kile unachofanya.

Kadiri unavyoweka umakini mkubwa kwenye chochote unachofanya, ndivyo unavyokifanya kwa kina na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufikia ubobezi.

Sheria Ya Leo; Siyo unayojifunza ndiyo yatakayozaa matunda, bali umakini mkubwa unaoweka katika kujifunza na kufanya ndiyo kutakufikisha kwenye ubobezi mkubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu