#SheriaYaLeo (74/366); Zama kwenye maelezo.

Kitu chochote kile unachotaka kubobea, unapaswa kuzama kwenye maelezo na kukijua kwa kina kabisa.
Kadiri unavyokijua kitu kwa kina, ndivyo unavyoona mengi na kuweza kukitumia kwa fursa kubwa.

Maelezo mengi ya kila kitu yanapatikana, kwa kuanzia ndani ya kitu hicho katika kukifanya na pia kwenye maarifa mbalimbali yaliyopo kuhush kitu hicho.

Kama hujui kwa kina kuhusu kitu siyo kwa sababu hakuna maelezo yake, ila ni kwa sababu hujaweka muda wa kutosha na kuzama kwa kina.
Kila anayekuzunguka anajua wazi kama unakijua kitu kwa kina au la.
Matokeo unayopata yanadhihirisha kama unajua kitu kwa kina au la.

Zama kwenye maelezo, jua kila kitu kwa kina na hakika mambo yako yatakwenda vizuri.
Kujifunza kwenye safari ya ubobezi huwa hakuna mwisho, endelea kujifunza kadiri unavyokwenda ili uzidi kufungua zaidi milango ya ubobezi zaidi.

Sheria ya leo; Gundua siri za kitu chochote kile kwa kuzama kwenye maelezo. Siri za vitu vyote zimefichwa kwenye maelezo, wanaozama huko ndiyo wanazijua siri hizo na kuweza kuzitumia vizuri.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji