Rafiki yangu mpendwa,
Ukimuona mtu yupo kwenye kilele cha mlima, unajua wazi kwamba mtu huyo hakuamka na kujikuta kwenye kilele hicho.
Bali alipanda mwenyewe kwenye kilima hicho, hatua kwa hatua.
Kadhalika unaposikia watu wamekula ng’ombe, haimaanishi wamempika ng’ombe huyo mzima mzima na kumla.
Bali ng’ombe huyo amechinjwa, akakatwa vipande vipande na ndiyo watu wakaweza kula vipande hivyo mpaka ng’ombe akaisha.
Hivyo ndivyo asili na maisha kwa ujumla yalivyo.
Kitu chochote kile kinaweza kufanyika na kufikiwa kwa kuchukua hatua ndogo ndogo kwa msimamo bila kuacha.
Lakini inapokuja kwenye mafanikio, wengi husahau msingi huo muhimu wa hatua ndogo ndogo.
Wengi hudhani ipo siri au njia ya mkato ya kuwawezesha kupata mafanikio makubwa kwa haraka.
Hiyo siyo kweli na wote ambao wamehangaika na mambo hayo wameishia kupoteza muda wao na nguvu zao na wasipate chochote.
Mafanikio makubwa kwenye maisha yanajengwa hatua kwa hatua.
Ni mambo madogo madogo yanayofanywa kwa kujirudia rudia ndiyo yanayoleta mafanikio makubwa.
Na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa siku moja unapokuja kwenye mafanikio.
Mafanikio kwenye maisha ni mkusanyiko wa siku nyingi ambazo mtu ameziishi kwa mafanikio.
Hiyo ina maana kwamba kama unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako, basi unapaswa kuhangaika na siku moja pekee.
Unapaswa kuipangilia vyema siku yako moja, kuyapa kipaumbele yale yaliyo muhimu na kuyafanya kwa viwango vya juu kabisa.
Ukishaiweza siku moja, kinachobaki ni wewe kurudia zoezi ulilofanya kwenye siku moja kuwa ndiyo unavyofanya kwenye siku zako zote.
Yaani unakuwa na kanuni yako ya kuiendesha siku yako na kisha unaifuata kanuni hiyo kila siku bila kuacha hata siku moja.
Na hapa najua unajiuliza unawezaje kutengeneza kanuni sahihi kwa siku yako? Yapi muhimu na yapi siyo muhimu?
Napenda kukupa taarifa kwamba maswali yako hayo yana majibu sahihi, yenye hatua za wewe kuchukua kwa uhakika ili kila siku yako iwe ya mafanikio na maisha pia yawe ya mafanikio.

Kitabu kipya cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ndiyo mwongozo sahihi kwako kwenye kuiishi kila siku yako kwa ukamilifu wake na kuweza kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha.
Usikubali tena kuzipoteza siku zako kwa kuhangaika na yasiyo na tija na ukajizuia kufanikiwa.
Pata leo nakala yako ya kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO uanze kuzidhibiti siku zako, ufanye makubwa kwenye kila siku yako na uweze kupata mafanikio makubwa.
Kitabu ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email au unaweza kukipata kwenye app ya SOMA VITABU.
Gharama ya kitabu kwa sasa ni kama zawadi, kwani unachangia tsh 4,500/= tu na unapata maarifa ya kina kabisa kukuwezesha kufanya makubwa kwenye kila siku yako.
Kukipata kitabu, tuma fedha na email yako kwenda namba 0678 977 007 (Amani Makirita) na kisha utatumiwa kitabu.
Pia unaweza kununua na kusomea moja kwa moja kwenye app ya SOMA VITABU, fungua; www.bit.ly/somavitabuapp
Rafiki, kutumia vizuri siku yako au kuipoteza ipo ndani ya uwezo wako kabisa.
Badala ya kuendelea kuhangaika na mbinu za mafanikio zinazopoteza siku yako ni wakati sasa wa kushika hatamu ya kila siku yako.
Pata leo na usome kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ili kiwe mwongozo mzuri kwako kutawala kila siku yako na kufanya makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini, Kocha Dr. Makirita Amani.