#SheriaYaLeo (76/366); Badili mtazamo wako.
Ubunifu ni matokeo ya kuwa muwazi na kuweza kukiangalia kitu kwa mitazamo mbalimbali.
Wakati wengine wanakiona kitu kwa mazoea, walio wabunifu huwa wanakiona kwa namna ya tofauti na ya kipekee.
Wanaona kitu kikiweza kutumika kwa namna tofauti na ilivyozoeleka.
Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kuwa ili uwe mbunifu na uweze kufikia ubobezi na mafanikio makubwa.
Using’ang’ane na mtazamo mmoja tu wa kitu kwa namna ilivyozoeleka.
Bali kuwa wazi kujenga mitazamo mingine na ya tofauti kwenye kila kitu.
Chimba kwa ndani na kuwa tayari kujaribu namna mpya za kufanya au kutumia kitu hata kama haijazoeleka hivyo.
Hakuna ubunifu ambao umewahi kutokana na mazoea.
Ubongo wa kila binadamu una nguvu kubwa ya ubunifu. Lakini nguvu hiyo itafunuliwa pale mtu anapoweza kuwa na mitazamo ya tofauti kwenye mambo mbalimbali.
Sheria ya leo; Ubunifu na mabadiliko ni vitu ambavyo haviwezi kutenganishwa. Angalia kila kitu kwa mitazamo tofauti na siyo tu kwa mazoea.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji