Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakueleza kuhusu kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.

Kila ninapotoa kitabu kipya, huwa napenda kila rafiki yangu akipate na kukisoma, maana nakuwa nimeweka maarifa mengi na sahihi kwa mtu kuweza kupiga hatua.

Na ili kila rafiki yangu aweze kupata kitabu hicho kipya, huwa nakitoa kama zawadi, kwa mtu kuchangia kiasi kidogo ili kukipata kitabu.

Kwa kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO unapaswa kuchangia tsh 4,500/= ili kukipata.
Na zawadi hiyo inaisha leo.
Hivyo nipende kutumia nafasi hii kukujulisha kama bado hujakipata kitabu hiki, chukua hatua sasa hivi ili zawadi hii isikupite.

Kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email au unaweza kukipata kwenye app ya SOMA VITABU.

Kukipata kitabu, tuma fedha na email yako kwenda namba 0678 977 007 (Amani Makirita) na kisha utatumiwa kitabu.
Pia unaweza kununua na kusomea moja kwa moja kwenye app ya SOMA VITABU, fungua; www.bit.ly/somavitabuapp

Rafiki, mwanafalsafa Seneca aliwahi kunukuliwa akisema; “Maisha ni marefu na muda ni mwingi kama mtu anajua jinsi ya kuutumia vizuri. Tatizo la muda siyo kwamba haupo wa kutosha, bali ni mwingi sana kiasi kwamba tunaupoteza kwa mambo yasiyo na tija”.

Rafiki, maneno hayo yaliyosemwa zaidi ya miaka elfu 2 iliyopita, yana ukweli mpaka leo.
Huhitaji kwenda mbali kuthibitisha hilo, bali unapaswa kuanza na wewe mwenyewe tu.

Si umekuwa unasema muda huna, mambo mengi na muda mchache. Sasa hebu fanya zoezi moja muhimu sana litakalokufumbua macho.

Chukua kalamu na karatasi, gawa karatasi kwenye pande mbili.
Upande mmoja wa karatasi orodhesha mambo yote uliyofanya siku ya jana, yote kabisa bila kuacha hata moja.
Upande wa pili andika malengo makubwa unayotaka kuyafikia.

Baada ya hapo oanisha yale uliyofanya na lengo ambalo yanasaidia kufikia.
Ukimaliza hapo, angalia ni mambo gani umefanya yanayochangia lengo na yapi ambayo hayachangii lengo.

Utajionea wazi jinsi ambavyo unahangaika na mambo mengi yasiyokuwa na tija kabisa. 
Utaona jinsi unavyochagua kupoteza muda wako mwenyewe.

Imetosha sasa, hupaswi kuendelea tena kupoteza muda wako wa siku. Ndiyo maana unahitaji sana kanuni ya kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa, ili uweze kuwa na maisha ya mafanikio.

Chukua hatua sasa hivi rafiki yangu kujipatia kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO kama zawadi nzuri ninayotoa kwako na uweze kunufaika na maarifa yaliyo ndani ya kitabu hicho.

Tuma sasa tsh 4,500/= kwenda namba 0678 977 007 (Amani Makirita) na kisha tuma ujumbe wenye email yako na utatumiwa kitabu.
Zawadi inaisha leo, baada ya leo kitabu kitakuwa kwa bei yake halisi ambayo ni ya juu kuliko hiyo.
Sitaki ukose zawadi hii rafiki yangu, hivyo chukua hatua sasa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini, Kocha Dr Makirita Amani.