2576; Marudio.
Kama hujawahi kuelewa hili basi nikusisitize tena, kila kitu kwenye maisha kinategemea sana marudio.
Hebu fikiria siku moja moyo wako ungesema umechoka kudunda na hivyo inabidi upumzike kwa siku chache.
Ni hakika hakutakuwa na maisha.
Kula, kupumua, kujifunza na hata kuchukua hatua ili ufanikiwe, inahitaji marudio yasiyo na ukomo na bila kuchoka.
Na ndiyo maana wale wanaopenda sana kile wanachofanya ndiyo wanaofanikiwa sana, kwa sababu wanakuwa tayari kurudia bila kuchoka.
Hatua ya kuchukua;
Kwa eneo unalotaka kufanikiwa sana, chagua vitu utakavyofanya kwa kurudia bila kuchoka na kuwa tayari kurudia kufanya kila siku.
Tafakari;
Ubobezi na mafanikio ni matokeo ya kurudia kufanya bila kuchoka.
Kocha.