Rafiki yangu mpendwa,
Aliyekuwa raisi wa Marekani Abraham Lincoln amewahi kunukuliwa akisema; “Baadhi ya watu wanapaswa kuwa matajiri ili kuwaonyesha wengine nao wanaweza kuwa matajiri na hilo linakuwa faraja kwa jamii nzima. Ambaye hana nyumba asibomoe nyumba ya mwenzake, bali afanye kazi kwa juhudi aweze kujenga nyumba yake.”
Rafiki, hayo ni maneno machache lakini yenye uzito sana katika eneo la mafanikio.
Hakuna sehemu nzuri na ya uhakika ya kujifunza mafanikio kama kutoka kwa wale ambao wameshafanikiwa.
Uwepo wao na mafanikio yao vinakuwa kichocheo kwako kufanikiwa pia.
Unaweza kuwa umetokea familia duni, hukupata elimu na hujawa na kazi yoyote ya uhakika. Kwa miaka mingi unaweza kuwa unaamini hicho ni kikwazo kwako kufanikiwa, na ukaona hilo ni kweli kabisa.
Lakini siku ukikutana na mtu aliyepitia hali kama zako, ametokea familia duni, hakupata elimu wala kuwa na kazi ya uhakika, ila amepambana na kufanikiwa, unagundua kumbe wewe ni mzembe tu.
Unapata hamasa na msukumo wa kushika hatamu ya maisha yako ili na wewe uweze kufanikiwa kama yeye. Maana unaona wazi kama yeye ameweza na wewe pia utaweza.

Hicho ndicho tunachokijenga kwenye KISIMA CHA MAARIFA, jamii ya tofauti kabisa ambayo inajifunza kutoka kwa wengine na kupambana kuwa bora.
Kuna kasumba mbaya kwenye jamii zetu ya watu waliofanikiwa kuchukiwa.
Watu hao wamekuwa wanaonekana ni wenye roho mbaya na wasiojali.
Mengi mabaya husemwa kuhusu watu hao kwa sababu wamechagua maisha ya tofauti.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunawapenda sana watu hao kwa sababu ndiyo wanaofungua njia zetu za mafanikio makubwa.
Hata kama hawatupi chochote kwenye mafanikio yao, kitendo tu cha wao kufanikiwa, ni msukumo tosha kwetu kufanikiwa pia.
Rafiki, napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha mahali ambapo utakutana na watu sahihi wanaopambana ili kufanikiwa.
Kwa kukutana na watu hao ana kwa ana utaondoka ukiwa na moto wa kwenda kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Sehemu hiyo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kama kuna kitu umekuwa unajiambia huwezi au hakiwezekani, umekuwa unajidanganya tu. Njoo kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 na utasikia hadithi za wengine ambazo zitakufanya uone jinsi umekuwa unajidanganya na hata kucheza kwenye hii safari ya mafanikio.
Utaondoka kwenye semina hiyo ukiwa na msukumo mkubwa wa kwenda kuweka juhudi kubwa na kufanya yale yote ambayo awali uliona huwezi.
Ninachoweza kukuambia kwa uhakika rafiki yangu ni hiki, chochote ambacho umekuwa unajiambia huwezi au hakiwezekani siyo kweli, kinawezekana sana, hujapata tu msukumo wa kutosha.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 inakwenda kukupa msukumo huo wa kufanya makubwa na kuweza kufanikiwa zaidi.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz