#SheriaYaLeo (89/366); Unganisha akili na machale.
Kadiri unavyozama kwenye kukifanya kitu, unapata uelewa wa ndani kabisa na kuweza kuona vitu ambavyo wengine hawaoni kirahisi.
Unakuwa na machale yanayokuwezesha kujua vitu ambavyo huwezi kuvielezea.
Unapata hisia fulani pale kitu kinapokuwa sahihi au siyo sahihi.
Unakuwa na uwezo wa kuiona dunia na kujua yanayoweza kutokea kwa kasi na usahihi mkubwa.
Unaweza kuona ndani zaidi na kung’amua siri kubwa za kile unachofanya.
Kwa kuunganisha uwezo huo mkubwa wa machale pamoja na uwezo wetu binadamu wa kufikiri, utaweza kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
Sheria ya leo; Unapounganisha akili na machale unakuwa na nguvu kubwa ya kuweza kuyaelewa mambo kwa undani na kufanya maamuzi sahihi. Yaendeleze maeneo hayo mawili kwa kuzama ndani kwenye ufanyaji.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji