#SheriaYaLeo (96/366); Jijenge Upya Kitabia.

Tabia ulizonazo na vile watu wanavyokuchukulia siyo kilema ambacho hakiwezi kubadilishwa.

Una nguvu ya kujijenga upya kitabia ili uweze kupata nguvu na madaraka ya kufika kule unakotaka kufika.

Mara nyingi tabia unazokuwa nazo na vile watu wanavyokuchukulia inakuwa kikwazo kikubwa kwako kufika kule unakotaka kufika.

Usikubali uwe kikwazo kwako mwenyewe kutokana na tabia na mazoea yako.
Jua ni vipi unapaswa kuwa ili upate unachotaka na kisha kuwa hivyo.

Unaweza kujibadili na kujijenga kwa namna yoyote ile unayotaka.
Hivyo jua kwa hakika unapaswa kuwa mtu wa aina gani, kisha chukua hatua kuwa mtu huyo ili upate unachotaka.

Sheria ya leo; Jijenge upya kitabia ili uweze kupata nguvu na mamlaka ya kupata na kufika kule unakotaka kufika. Kujijenga kwa namna bora ndiyo kazi yako kuu katika kupata kile unachotaka kwenye maisha. Ipe kazi hiyo kipaumbele sahihi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji