#SheriaYaLeo (103/366); Watumie Maadui Zako.

Haijalishi unafanya nini, kuna watu ambao hawatakubaliana na wewe.
Watakuona ni mbaya, hufai na watatangaza uadui na wewe.

Kwa hali ya kawaida ya kibinadamu na wewe utasukumwa kutangaza nao uadui.
Ila jua kufanya hivyo hakuna manufaa kwako au kwao.
Mtasumbuana bila ya kuwa na manufaa yoyote.

Badala ya kujenga uadui na maadui zako, wewe jenga nao urafiki.
Jua maslahi yao na onekana kama unawapa kile wanachotaka.
Jenga nao ukaribu na wafanye waone wana wajibu wa kufanya mambo mazuri kwako.

Kwa njia hiyo utakuwa umepunguza uadui na kutopoteza nguvu zako kuhangaika na mambo yasiyo na tija.

Kumbuka binadamu ni binadamu, inapokuja kwenye maslahi binafsi, uadui huwekwa pembeni.

Adui uliyemfanya rafiki huwa mwaminifu kuliko hata rafiki uliyekuwa naye.
Maana anajua anatakiwa kuthibitisha kwamba hana uadui tena.

Waswahili waliposema mchawi mpe mwanao akulele, waliona mbali. Atafanya kila kitu kumlinda kwa sababu anajua akidhurika yeye ndiye ayakayeshutumiwa.

Sheria ya leo; Njia rahisi na bora ya kummaliza adui ni kumfanya awe rafiki. Atahangaika yeye mwenyewe kujenga uaminifu kwako kitu ambacho kitakuweka wewe salama zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji