2620; Matumaini na uhakika.
Watu huona matumaini kama kitu cha kujifurahisha, ambacho siyo uhalisia.
Hupenda zaidi uhakika kwenye kila jambo.
Lakini ukweli ni kwamba katika hali ya kawaida, kuujua ukweli ni vigumu sana.
Hivyo kujipa uhakika kabla hujaujua ukweli ni kujiweka kwenye hatari kubwa, kuwa kikwazo kwako mwenyewe kupiga hatua.
Kwa pale ulipo sasa unaweza usiione njia ya kwenda kule unakotaka kufika.
Kama unaamini zaidi kwenye uhakika utaona huo ndiyo mwisho, hakuna tena njia.
Lakini huo siyo ukweli, kwa sababu huioni njia haimaanishi kwamba haipo.
Unapoamini kwenye matumaini, unaendelea kwenda, japo huoni njia yote. Unasonga mbele kwenye ile njia fupi iliyo mbele yako.
Na unaendelea kupiga hatua hivyo, mpaka unajikuta umefika ulikotaka kufika.
Kilichokufikisha siyo uhakika wa njia, bali matumaini kwamba njia ipo.
Matumaini ni muhimu na yana nguvu kubwa sana, usikubali mtu yeyote ayavunje matumaini yako, hata kama atakupa ushahidi wa aina gani.
Maana ukweli ni mgumu sana kufikiwa.
Kadhalika usiwe mtu wa kuvunja matumaini ya wengine.
Hata kama kwa nje huoni namna kile wanachotaka kinawezekana, jua kuna mpaka nafasi ya bahati, ambayo huwezi kuiona kabla.
Matumaini ndiyo nguvu kuu inayoendesha maisha, hayo yakikosekana, maisha yanakosa kabisa maana.
Hatua ya kuchukua;
Jijengee matumaini makubwa kwenye mafanikio makubwa unayoyataka.
Hata kama mbele unaona giza kabisa, usipoteze matumaini kwamba utapata unachotaka.
Na matumaini yako yasiwe ndiyo kitu pekee unachotegemea, bali yatumie kupata msukumo wa kukaa kwenye mchakato, kuendelea kuchukua hatua kwenye kile unachotaka.
Tafakari;
Napoleon amewahi kunukuliwa akisema kiongozi ni muuza matumaini. Na hilo ni sahihi kabisa, kitu pekee ambacho kiongozi ana ukakika nacho ni maono makubwa aliyonayo. Jinsi ya kuyafikia hakuna uhakika wowote, lakini anapowauzia watu matumaini, wanafanya kila namna kuyafikia maono hayo.
Kocha.
Asante sana kocha wewe ni kiongozi wetu kutupa matumaini.Matumaini ndiyo ya muhimu sana kutuwezesha kukaa na mchakato hata pale ambapo hatuoni mbeleni kukoje.
LikeLike
Asante sana.
LikeLike
Matumaini. Kuna Hadi bahati ambayo haionekani…Ni kila siku huwa unanitafakarisha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike