#SheriaYaLeo (125/366); Usidanganyike na mwonekano wa nje.

Mara nyingi watu wamekuwa wanatengeneza mwonekano fulani wa nje ambao unaficha nia yao halisi.

Kwa nje wanaigiza kama wajinga na wasiojua vitu fulani.
Lengo lao ni kuwahadaa watu ili wasijue nia zao na kuwa kikwazo kwao.

Wewe kuwa makini, usikimbilie kuamini mwonekano wa nje wa watu.
Badala yake jua kila mtu ana nia fulani ndani yake ambayo hataki kuiweka wazi.

Utakuwa upande salama zaidi kama utachukulia kila mtu kama mwenye nia ya ndani ambayo haiweki wazi kwa nje.

Kwa namna hiyo hutaingia kirahisi kwenye mitego ambayo wanaiweka ili kukuhadaa na wapate kile wanachotaka.

Kuwa makini, wanaoonekana wajinga kwa nje, ndani wanajua kwa hakika nini wanataka.
Mwonekano wao wa ujinga ni mbinu ya kuwahadaa watu wasiwe kikwazo kwao.

Na kama ambavyo tumekuwa tunajifunza mara kwa mara kupitia sheria hizi, kile ambacho watu wanatumia nguvu kubwa kukionyesha kwa nje, huwa ni kinyume na uhalisia ulio ndani yao.
Hili ni jambo muhimu sana la kujua na kuzingatia wakati wote ili usihadaike kirahisi na mbinu mbaya za wengine.

Sheria ya leo; Wale wanaojionyesha kwa nje kwamba hawana hatia, ndiyo wenye hatia kubwa. Usidanganyike na mwonekano wa nje, ndani ya watu kuna mengi kuliko yanayoonekana kwa nje.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji