2666; Umetingwa na yapi?

Kutingwa au kuwa bize kama wengi walivyozoea kutumia ndiyo kuna nguvu kubwa ya kuamua matokeo ambayo mtu anayapata kwenye maisha yake.

Kile kinachokuweka bize ndiyo kinachozalisha matokeo kwenye maisha yako.

Matokeo unayopata sasa, iwe ni mazuri au mabaya yamezalishwa na yale yaliyokutinga huko nyuma.

Usilaumu watu kwa matokeo unayopata, maana umeyaandaa wewe mwenyewe.

Kama waswahili wanavyosema mtu unavuna ulichopanda, huwezi kuweka muda na nguvu zako kwenye jambo fulani halafu utegemee matokeo tofauti.

Hatua ya kuchukua;
Pitia yale unayofanya kila siku.
Angalia ni mambo gani yanayokuweka bize zaidi.
Jua hayo ndiyo yanayotengeneza matokeo unayopata.
Kama upo bize na mambo yasiyo na tija, jua utazalisha matokeo yasiyo na tija.

Tafakari;
Hakuna kinachotokea kama ajali.
Kila kinachotokea kimesababishwa.
Badala ya kulalamikia matokeo, jiulize umeyasababishaje na utaweza kuyabadili.

Kocha.