#SheriaYaLeo (178/366); Kamwe usifanye kwa mazoea.
Unapokuwa kijana huwa ni rahisi kuchukua hatua za tofauti.
Japo zinaweza kuwa hatari, lakini ndiyo zinazoleta matokeo makubwa na ya tofauti.
Lakini kadiri umri unavyokwenda, unaanza kufanya zaidi kwa mazoea badala ya kujaribu vitu vipya.
Kutokana na umri kwenda, unaepuka hatua ambazo ni hatari na kufanya yale ambayo umeshayazoea na yana uhakika.
Hapo ndipo anguko la wengi linapoanzia.
Kutokuchukua hatua za hatari ndiyo hatari kubwa kuliko zote kwenye maisha.
Kufanya yale ambayo umeshayazoea na yanayokupa matokeo ya uhakika ni kujizuia kupata matokeo makubwa na ya tofauti.
Pia inakufanya uwe unatabirika kirahisi kitu kinacholeta vikwazo zaidi kwako.
Usikubali kabisa kurudi kwenye mazoea.
Hata pale unapokuwa umefanikiwa, usifanye kile ulichozoea kwa kuhofia hatari.
Utakuwa unajiweka kwenye nafasi ya kuanguka.
Endesha vita ya kuondoa mazoea kwenye maisha yako.
Haijalishi umefika wapi, kila wakati chukua hatua mpya na za tofauti.
Ni kupitia hatua hizo ndiyo unaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako na kuzidi kubaki kwenye kilele cha mafanikio.
Sheria ya leo; Jenga tabia ya kuvunja mazoea yako na kufanya vitu ambavyo ni vya tofauti. Chukua hatua mpya na za hatari ili kuweza kupata matokeo makubwa na ya tofauti. Kamwe usifanye chochote kwa mazoea.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji