#SheriaYaLeo (180/366); Tengeneza upya nguvu ya mamlaka yako.

Unaweza kujenga mamlaka yako au mafanikio na kufika viwango vya juu kabisa.

Lakini kadiri muda unavyokwenda, mamlaka hayo yanaanza kupoteza nguvu zake.

Watu wanakuzoea kwa yale ambayo tayari umekuwa unayafanya.
Na huku watu wapya wanaokuja wakiwa hawakujui vyema.

Wewe mwenyewe unakuwa unafanya mambo yako kwa mazoea kiasi kwamba ni rahisi watu kukutabiri.
Na ikishakuwa rahisi kwa watu kukutabiri, ile heshima na hofu yao kwako inakuwa haipo tena.

Ili kuondokana na hali hizo, kila wakati unapaswa kutengeneza upya nguvu ya mamlaka yako.

Haijalishi upo juu kiasi gani, usifanye kwa mazoea.
Badala yake kila wakati fanya vitu vipya vinavyoimarisha mamlaka na mafanikio yako.

Fanya vitu ambavyo watu hawajavizoea kwako.
Pambana kuwafikia watu wapya na tofauti kabisa na wale ambao tayari wanakujua.

Juhudi hizo zitakufanya uendelee kuwa juu na mamlaka yako kuwa kubwa wakati wote.

Kadiri unavyokaa kwenye mamlaka au mafanikio kwa muda mrefu ndivyo unavyozoeleka na kuchukuliwa wa kawaida.
Watu wanapenda vitu vipya na vya tofauti, wape hivyo na utabaki kileleni wakati wote.

Sheria ya leo; Kuwa tayari kubadilika na kujaribu vitu vipya kunakupa nguvu ya kubaki kwenye nafasi kubwa uliyofikia. Kunakuwezesha kufanikiwa zaidi na kuimarisha mamlaka uliyonayo. Kamwe usipoteze uwezo huo hata kama umefika juu kiasi gani.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji