#SheriaYaLeo (183/366); Iangalie dunia kwa jicho la ushawishi.

Ili kuweza kuwa na nguvu ya ushawishi huhitaji kuwa na mabadiliko makubwa kwenye tabia au mwonekano wako.

Ushawishi ni mchezo wa kisaikolojia na hivyo kila mtu anaweza kuwa na ubobezi kwenye mchezo huu.

Kinachohitajika ni uiangalie dunia kwa utofauti, kupitia jicho la ushawishi.
Unapaswa kuiona dunia kama sinema na kila mtu kama mwigizaji.

Watu wengi hujichukulia kama wana nafasi na majukumu yaliyofungwa kwenye maisha, kitu kinachowakosesha furaha.

Wenye ushawishi wanajua wanaweza kuigiza nafasi yoyote kwa wakati wowote. Anaweza kuigiza nafasi nyingi kwa wakati mmoja.

Wenye ushawishi huwa wanafurahia kucheza nafasi hizo mbalimbali na hawasumbuki na hali ya kuona lazima wawe kwa namna fulani waliyozoeleka.

Ni huo uwezo na utayari wao wa kubadilika ndiyo unawafanya watu wavutiwe kwao na kushawishika nao.

Ili kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine lazima uwe tayari kubadilika kila mara, kuendana na vile watu wanataka.

Kama tunavyojua, ukweli huwa unauma na wengi huwa hawapo tayari kuupokea ukweli.
Hivyo ili kuwa na ushawishi, usiwaambie watu ukweli, bali kile wanachotaka kusikia au kuona.
Na ndiyo maana mwenye ushawishi anapaswa kuwa tayari kubadilika muda wote.

Sheria ya leo; Ushawishi ni aina ya sinema kwenye maisha, kukutana kwa udanganyifu na uhalisia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji