Rafiki yangu mpendwa,

Kitu ambacho watu wengi huwa hawajui ni kwamba utajiri au umasikini ni matokeo.

Na kisababishi cha matokeo hayo huwa ni tabia ambazo mtu anakuwa nazo.

Ninachomaanisha ni kwamba hakuna mtu anayezaliwa tajiri au masikini.

Bali kila mtu hutengeneza utajiri au umasikini kutokana na tabia anazokuwa nazo.

Ndiyo maana kuna watu wamezaliwa kwenye umasikini mkubwa ila wakaishia kuwa matajiri.

Na wapi watu waliozaliwa kwenye utajiri mkubwa ila wakaishia kuwa masikini.

Siyo bahati au ajali, bali ni matokeo ya tabia.

Na kama wanavyosema, huwa tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga.

Hivyo kama unataka kutoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri, hapa kuna TABIA 17 unazopaswa kuzibadili kwenye maisha yako.

Tabia hizi zipo kwa picha rahisi kuelewa, hivyo hata kama kusoma kunakupa shida basi angalia picha hizi na ujifunze.

1. Matajiri wanaamini wao ndiyo wamejitengeneza wenyewe na hivyo kuchukua wajibu wa maisha yao. Lakini masikini wanaamini maisha waliyonayo yametengenezwa na wengine na hakuna wanachoweza kufanya kuyabadili.

2. Matajiri huwa wanacheza mchezo wa fedha ili kushinda, yaani kufika kwenye utajiri mkubwa. Wakati masikini huwa wanacheza mchezo wa fedha ili kutokupoteza, yaani wanachotaka ni kuwa na usalama.

3. Matajiri huwa wamedhamiria na kujitoa kweli ili kufikia utajiri, hawakubali chochote kiwazuie kufikia utajiri. Wanakuwa wameyatoa maisha yao yote kwa lengo la kufikia utajiri na hapo dunia inakuwa haina namna bali kuwapa utajiri wanaotaka. Masikini huwa wanatamani kufika kwenye utajiri, lakini wanakuwa hawajajitoa kweli. Wanakuwa na zile ndoto za kulala masikini na kuamka tajiri au kukutana na ‘zali la mentali’. Ni rahisi kuyumbishwa na kuondoka kwenye matakwa yao ya utajiri na hivyo huwa hawafiki kwenye utajiri.

4. Matajiri huwa wanafikiri kwa viwango vikubwa na hilo linawapelekea kupata matokeo makubwa. Lakini masikini huwa wanafikiri kwa viwango vidogo na kuishia kupata matokeo madogo. Kanuni ya kipato inasema; unalipwa kulingana na thamani unayotoa kwa wengine. Hivyo unapotoa thamani kubwa na kuitoa kwa wengi, ndivyo malipo unayopata yanavyokuwa makubwa.

5. Katika kitu kimoja, masikini na matajiri wana mtazamo tofauti. Matajiri wanaona fursa wakati masikini wanaona vikwazo. Matajiri wanaona nafasi ya kukua zaidi wakati masikini wanaona nafasi ya kupoteza. Matajiri wanaangalia upande wa faida, wakati masikini wanaangalia upate wa hatari na hasara. Unapaswa kubadili mtazamo na imani yako, uache kuona vikwazo na uanze kuona fursa nzuri zilizopo kwenye kila jambo.

6. Matajiri huwa wanawapenda na kuwakubali matajiri wengine, hasa waliowazidi utajiri. Kwa kufanya hivyo wanakuwa tayari kujifunza kwao na kuweza kutajirika zaidi. Masikini huwa wanawachukia na kuwakataa matajiri na wote waliowazidi kipato. Huwachukulia ni watu waovu na wasiojali. Kwa kufanya hivyo wanakuwa hawapo tayari kujifunza kutoka kwa waliowazidi na hivyo kuendelea kubaki kwenye umasikini. Huwezi kupata kile unachokichukia, hivyo ukiwachukia matajiri ni uhakika kwamba huwezi kuwa tajiri.

7. Matajiri huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mtazamo chanya na waliofanikiwa. Watu wanaoamini kwenye uwezekano na wanaohamasisha na kutoa matumaini. Masikini huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mtazamo hasi na walioshindwa. Watu waliokata tamaa na wanaoamini haiwezekani na wanaoondoa matumaini.

8. Matajiri huwa wanajitangaza na kujiuza kwa wengine, kwa kuwa tayari kueleza kile wanachofanya na kuwashawishi wengine kukipata. Kwa njia hii matajiri hujulikana zaidi, hupata wateja wengi na kuuza zaidi. Masikini huwa hawajitangazi wala kujiuza, huwa wanaona aibu kufanya hivyo na kuona wanaojitangaza wanatafuta tu sifa. Kwa njia hiyo masikini hawajulikani na wengi na hivyo hawapati wateja wengi na mauzo yao huwa ni kidogo.

9. Matajiri huwa wanayazidi matatizo yao, wanakuwa wakubwa kuliko matatizo hayo na hivyo hayawatishi, wanayatatua na kusonga mbele. Masikini huwa wanazidiwa na matatizo yao, wanakuwa wadogo kuliko matatizo hayo na hivyo yanawatisha na wanashindwa kuyatatua.

10. Matajiri huwa wanapokea vizuri kila wanachopata, wanajua wanastahili kupata na wanashukuru kwa kukipata. Masikini huwa hawapokei vizuri kile wanachopata, wanajiona hawastahili na hawashukuru kwa kupata.

11. Matajiri huwa wanachagua kulipwa kwa matokeo wanayozalisha na hapo wanazalisha matokeo makubwa zaidi na kulipwa kiasi kikubwa cha fedha. Masikini wanachagua kulipwa kwa muda wanaotumia kufanya kitu na kwa kuwa muda una ukomo, wanajiwekea ukomo kwenye kipato chao.

12. Matajiri huwa wanaamini wanaweza kupata vyote kwa pamoja, yaani utajiri na vitu vingine vizuri kwenye maisha kama furaha, upendo na amani. Na hivyo ndivyo maisha yao yanavyokuwa, wanakuwa matajiri wenye furaha, amani na upendo. Masikini huwa wanaamini hawawezi kupata vyote kwa pamoja, wakipata kimoja basi wamekosa kingine. Wanaamini wakipata utajiri hawawezi kuwa na furaha, amani na upendo. Kinachotokea ni wanakosa vyote, hawapati utajiri na bado maisha yao hayawi ya furaha.

13. Matajiri huwa wanaweka mkazo kwenye ukubwa wa utajiri wao na hilo hupelekea utajiri wao kukua zaidi na zaidi. Masikini huwa wanaweka mkazo kwenye ukubwa wa kipato chao na hilo huwa kikwazo kwao kufikia utajiri. Kipimo sahihi cha utajiri ni thamani ya utajiri ambao mtu anao, unaohusisha kila kitu anachomiliki. Kipato ambacho mtu anaingiza pekee siyo kipimo cha utajiri, ni sehemu tu.

14. Matajiri huwa wanasimamia fedha zao vizuri, hawaachi mianya ya kupelekea wapoteze fedha zao. Masikini huwa hawasimamii fedha zao vizuri, wanaacha mianya mingi inayopelelea kupoteza fedha. Ili ufikie utajiri unapaswa kuzidhibiti fedha na siyo fedha kukudhibiti wewe. Na ili kuweza kuzidhibiti fedha lazima uweze kuzisimamia vizuri.

15. Matajiri huwa wanazifanya fedha zao ziwafanyie kazi, ziwatumikie. Hapo wanakuwa na njia ya kufanya fedha zao zizalishe faida hata kama wamelala, wanakuwa na njia ya kuingiza kipato bila kufanya kazi moja kwa moja. Masikini wanazifanyia kazi fedha zao, fedha zinawatumikisha. Hawana mfumo wa kuingiza kipato bila kufanya kazi na hivyo wanalazimika kufanya kazi kila wakati ndiyo waweze kupata fedha.

16. Matajiri huwa wanachukua hatua licha ya kuwa na hofu, wanajua njia ya kuishinda hofu ni kufanya kile wanachohofia. Ni kwa njia hiyo wamekuwa wanazalisha matokeo makubwa na ya tofauti kabisa. Masikini wamekuwa wanaruhusu hofu iwe kikwazo kwao, wanapopanga kuchukua hatua na hofu ikawajia, wanaacha kufanya.

17. Matajiri huwa wanajifunza kila siku na kuendelea kukua. Hakuna wakati wanajiona wameshajua kila kitu, wanajua kuna mengi hawajui na hivyo kuwa wanyenyekevu na kujifunza. Masikini huwa hawajifunzi kila siku, wakishahitimu masomo wanaamini tayari wanajua kila kitu. Kwa njia hiyo hawakui kwa sababu kuna mengi hawajui ambayo yanakuwa kikwazo kwao.

Je ungependa kujifunza kwa kina kuhusu TABIA bora za kujijengea ili uweze kufikia utajiri mkubwa kwenye maisha yako?

Nina habari njema kwako, kitabu kipya cha TABIA ZA KITAJIRI kimesheheni maarifa sahihi ya kukuwezesha wewe kujijengea tabia ambazo zitakuondoa kwenye umasikini na kukufikisha kwenye utajiri mkubwa.

Ni tabia ambazo kila mtu anaweza kujijengea na zikawa na manufaa makubwa kwake. Hivyo hata wewe ni tabia ambazo zitakuwa na manufaa kwako.

Karibu sana usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako, kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

JINSI YA KUPATA KITABU CHA TABIA ZA KITAJIRI.

Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo.

Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.

Kujipatia nakala yako ya kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.

ZAWADI YA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu, nakwenda kukupa kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utakipata kitabu hiki kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh elfu kumi na tano (15,000/=), badala ya bei yake halisi ambayo ni tsh elfu 20

Kitabu hiki kina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unakipata sawa na bure kabisa, kwa tsh elfu 15 tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kukikosa, kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu, zawadi hii ni ya muda mfupi, bei ya kitabu itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia. Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.

Kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI kina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, wasiliana na 0752 977 170 kukipata kitabu popote pale ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.