#SheriaYaLeo (209/366); Jua wakati sahihi wa kuwa jasiri.

Hakuna mtu yeyote anayezaliwa akiwa muoga.
Woga ni tabia ambayo tunajifunza kwenye maisha ili kujilinda.

Woga unatuaminisha kwamba kama hatutafanya yale yanayofanya tuonekane, kama hatutajaribu mapya na makubwa, basi hatuwezi kusumbuliwa na matokeo ya kufanikiwa au kushindwa.

Huwa tunaamini kama tukiwa wema na tusiokuwa na vipingamizi kwa wengine, hakuna tutakayemkasirisha na hapo tutaonekana watakatifu na kupendwa na kila mtu.

Lakini huo siyo ukweli kwenye uhalisia.
Woga unaweza kuwa na matumizi ya aina mbalimbali, lakini kamwe hauna ushawishi.
Huwezi kuwashawishi wengine kwa kutumia woga.
Bali unaweza kuwashawishi wengine kwa kutumia ujasiri.

Unapaswa kuweza kuigiza unyenyekevu na utakatifu pale inapohitajika. Hiyo ni kama barakoa unayoweza kuvaa pale inapohitajika.
Lakini inapokuja kwenye ushawishi, lazima uvue barakoa hiyo na kuvaa hali ya ujasiri.

Watu huwa wanawakubali zaidi watu wenye ujasiri kwa sababu wanakuwa wameonyesha kile ambacho hata wao wangependa sana kukionyesha ila wamekosa uthubutu.
Wanapoona mwingine ameonyesha uthubutu, wanaona na wao pia wanaweza kuonyesha uthubutu pia.

Sheria ya leo; Katika hatua za mwisho za ushawishi, ujasiri unaondoa wasiwasi wowote ambao mtu anakuwa nao.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji