#SheriaYaLeo (211/366); Kumshawishi anayetaka kukushawishi.

Kuna wakati unajikuta kwenye hali ambapo unahitaji kumshawishi mtu ambaye na yeye pia anataka kukushawishi.

Hapo unapaswa kutumia mbinu ya kumwonyesha kitu au tabia ya kutaka kushawishika naye.

Yaani unamrahisishia zoezi lake la kukushawishi wewe, kitu ambacho kinakuwa rahisi kwako kumshawishi yeye pia.

Unapomnasa mtu kwenye mtego wa kukushawishi, inakuwa rahisi kwako kumshawishi pia.

Onekana kushawishika na mtu ili na yeye aweze kushawishika na wewe.

Sheria ya leo; Tengeneza picha ya kushawishika na wengine ili kuwashawishi kirahisi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UdadisiUpekeeUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji