Jinsi Ya Kuidhibiti Siku Yako Ili Uweze Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa,

Mambo kuwa mengi huku muda ukiwa mchache ndiyo malalamiko makubwa kwa kila mtu kwenye zama tunazoishi sasa.

Siku zimekuwa fupi kweli kweli, kunakucha na ukija kushtuka, siku imeisha, umechoka na ukiangalia hakuna kikubwa ambacho umefanya.

Siku zinayoyoma, mwaka unaanza na kuisha na bado mtu unajikuta unabaki pale pale.

Unaweza kuwa na malengo na mipango mikubwa ya kufanikiwa kwenye maisha. Ila tatizo ni kupatikana kwa huo muda wa kufanyia kazi hayo malengo na mipango.

Kwani kila siku inaisha na muda haupatikani, kila siku umetingwa na huwezi kufanya yale ambayo ni muhimu.

Changamoto hii inazidi kuwa kubwa kadiri muda unavyokwenda, kwa sababu mambo ya kufanya yanaongezeka mara dufu, lakini muda wetu kwenye siku ni ule ule, masaa 24.

Ni katika kutafiti namna ya kuvuka kikwazo hicho na kuweza kufikia mafanikio tunayoyataka ndiyo nimefanikiwa kukuandalia kitabu kipya kinachoitwa; KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kuidhibiti Siku Yako Ili Uweze Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yako.

Rafiki, hiki ni kitabu sahihi kwako na ambacho kimekuja kwa wakati sahihi kwako, kwani mafanikio yoyote unayoyataka kwenye maisha yako, yanajengwa na namna unavyoziishi siku zako.

Haijalishi unataka kufika wapi, hutajikuta tu umefika kwa ajali au bahati, bali ni hatua unazopiga kila siku ndiyo zitakufikisha kokote unakotaka kufika.

Jinsi unavyoiishi siku yako moja ndiyo unavyoziishi siku zako nyingi na hilo ndiyo litakaloamua ufanikiwe au usifanikiwe.

Kwa maneno mengine ni kwamba, ukinipa nafasi ya kukufuatilia kwenye siku yako moja kwa kawaida, naweza kutabiri kwa usahihi wa zaidi ya asilimia 90 kama utafanikiwa au la.

Hiyo ni kwa sababu sisi binadamu ni viumbe wa kitabia, vitu vingi unavyofanya kwenye siku yako ndiyo tabia yako. Kama ndiyo tabia yako utaendelea kuirudia, hivyo siku zako nyingi zitafanana. Sasa kama tabia ulizonazo siyo nzuri, huhitaji kupiga ramli ili ujue ni matokeo gani yatapatikana kwenye maisha ya aina hiyo.

Rafiki, sasa unaweza kuwa mtabiri mzuri wa maisha yako mwenyewe, kuamua kama ufanikiwe au la, kwa kuchagua namna unavyoiishi siku yako moja na kurudia siku hiyo kila siku.

Kitabu cha KANUNI YA MAISHA YA MAFANIKIO kimekuja kukupa ukombozi wa kuweza kumiliki na kudhibiti siku zako na kutumia siku hizo kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Kwenye utangulizi wa kitabu hiki utajifunza jinsi ambavyo mafanikio makubwa ya maisha yako yanategemea jinsi unavyoiishi siku yako moja. Hapa utajifunza dhana ya mafanikio ni kila siku na siyo siku moja unayotegemea kufika kileleni. Kwa kuweza kuiishi kila siku kwa mafanikio, siku hizo zitakusanyika na kuwa maisha ya mafanikio.

Sura ya kwanza ya kitabu ni asubuhi ya miujiza. Hapa unajifunza jinsi unavyoweza kuidhibiti asubuhi yako na kuitumia kufanya mambo ambayo yatakufikisha kwenye mafanikio makubwa. Kwenye sura hii utajifunza mambo sita ambayo ukiweza kuyafanya kila siku asubuhi lazima ufanikiwe. Uzuri ni kwamba, unaweza kufanya mambo hayo sita kwa dakika sita tu. Ndiyo, DAKIKA 6!

Sura ya pili ni kuhusu klabu ya saa kumi na moja alfajiri. Unaijua usemi wa Waswahili unaosema; nyota njema huonekana asubuhi. Na mwingine unasisitiza; biashara ni asubuhi, jioni mahesabu. Kwenye sura hii utajifunza jinsi asubuhi na mapema ilivyo na nguvu kwenye siku yako na maisha yako kwa ujumla. Kwa kuweza kuamka mapema na kutenga saa moja kwa ajili yako, utaleta mapinduzi makubwa sana kwenye maisha yako.

Sura ya tatu ni kuhusu kujenga tabia bora za kuiishi siku yako kwa mafanikio ili uwe na maisha ya mafanikio. Hapa utajifunza hatua nne za kujenga tabia ambayo itadumu na kuwa na manufaa kwako. Na kama una tabia ambayo ni kikwazo, pia utajifunza jinsi ya kuivunja kwa hatua hizo hizo nne.

Sura ya nne inahusu kupata utulivu kwenye siku yako. Tunaishi zama ambazo zina usumbufu na kelele za kila aina. Huhitaji hata kwenda mbali ndiyo ukutane na usumbufu huo, kwani simu yako tu ni chanzo tosha cha usumbufu. Kwenye sura hii utajifunza nguvu kubwa iliyopo kwenye utulivu na jinsi ya kuitumia kuwa na siku bora na maisha yenye mafanikio.

Sura ya tano inajumuisha kwa pamoja yale uliyojifunza na kutengeneza kanuni sahihi ya siku ya mafanikio. Kanuni hiyo ina vipengele vitatu, kudhibiti asubuhi yako, kushinda mchana wako na kuweka umakini kwenye jioni yako. Kwenye sura hii utajifunza mambo ya kufanya asubuhi, mchana na jioni ili siku yako iwe ya mafanikio makubwa.

Hitimisho la kitabu litakupa mtazamo wa kifalsafa zaidi, mtazamo utakaokufanya ufikiri kwa tofauti na kuona ukomo mkubwa uliopo kwenye muda. Sura hiyo ina swali vipi kama leo ndiyo siku yako ya mwisho kuwa hapa duniani? Je utaitumia siku yako ya mwisho kuperuzi mitandao, kuhangaika na habari au kuwachukia wengine? Jibu ni hapana, siku yako ya mwisho utautumia muda vizuri, maana ni wa thamani sana. Hitimisho hilo la kitabu litakupa mtazamo wa namna ya kuishi kila siku yako kama siku ya mwisho na kuweza kufanya makubwa.

Rafiki, kitabu hiki cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO siyo cha wewe kukosa, kwani kimekuja kama mkombozi wako kwenye changamoto kubwa tunayopitia sasa ya mambo kuwa mengi huku muda kuwa mchache.

JINSI YA KUPATA KITABU.

Kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy).
Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo.
Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.

Kujipatia nakala yako ya kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.

ZAWADI YA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu, nakwenda kukupa kitabu hiki cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utakipata kitabu hiki kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh elfu kumi na tano (15,000/=), badala ya bei yake halisi ambayo ni tsh elfu 20

Kitabu hiki kina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unakipata sawa na bure kabisa, kwa tsh elfu 15 tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kukikosa, kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu, zawadi hii ni ya muda mfupi, bei ya kitabu itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Kushika hatamu ya maisha yako ni hitaji muhimu sana kwako kama unataka kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha.

Kitabu hiki cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO kina kanuni za kukuwezesha wewe kushika hatamu ya maisha yakk, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na uweze kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, hii ni nafasi ya kipekee kwako kwenda kurudisha utawala na ushindi kwenye siku zako ili kuweza kujenga maisha yenye mafanikio makubwa. Jipatie sasa kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO kwa kutumia njia hizo hapo juu na uweze kuyabadili maisha yako.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, wasiliana na 0752 977 170 kukipata kitabu popote pale ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.